Kwa karne kadhaa sasa kumekuwa na hofu, gumzo na minong’ono juu ya mitandao inayoendesha siasa za Ulimwengu kwa siri. Mitandao hiyo ni Freemansory na Mafyay ambayo yote iko chini ya nguvu za uzayuni wa kimataifa. Kitabu hiki kimejaribu kuielezea mitandao hiyo zaidi kikiwa kimejikita katika ule mashuhuri wenye jina la “Freemasonry” au kwa utohozi usiyo rasmi “Frimansori”. Mtandao huu umejengwa na watu walioamua kujitoa muhanga wenye kuzingatia miiko na tahadhari zote ili kufanikisha lile walilolikusudia. “Frimansonri” ni tafsiri inayogeuza kidogo matamshi, inatanguliza n kabla ya s na kisha n. Freemansonry-Frimansori. Katika kitabu hiki tutatumia tafsiri hii pamoja na neno Mafya.